Matthew 1:21-25

21 aNaye atamzaa mwana, nawe utamwita Jina lake Isa,
Isa ni Iesous kwa Kiyunani, na kwa Kiebrania ni Yoshua au Yeshua. Maana yake ni Yehova ni wokovu.
kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao.”

22 cHaya yote yalitukia ili litimie lile Bwana alilokuwa amenena kupitia nabii, akisema: 23 d“Tazama, bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, nao watamwita Jina lake Imanueli”: maana yake, “Mungu pamoja nasi.”

24 eYusufu alipoamka kutoka usingizini, akafanya kama vile alivyoagizwa na malaika wa Bwana, akamchukua Mariamu kuwa mke wake. 25 fLakini hawakukutana kimwili mpaka Mariamu alipojifungua mwanawe kifungua mimba akamwita Jina lake Isa.
Copyright information for SwhKC